Friday, June 15, 2018

SHUKRANI NA KUSITISHA MATANGAZO NA MACHAPISHO YETU RASMI

G SAMBWETI


Kwanza uongozi mzima wa G SAMBWETI blog  unatoa shukrani za dhati kwa wale wote waliowahi kutembelea blog hii ambao ni  watu zaidi ya laki nane elfu thelathini mia  tatu na arobaini na tatu (833343) tangu ilipoanzishwa hapo mwaka 2011 hadi  leo 15/06/2018

hatuna budi kuwashukuru sana kwani nilipenda kuendelea kuwahabarisha bali sheria za TCRA zinanilazimu  kusitisha  uchapishaji  katika gazeti lenu hilipendwa la  G sambweti blog.

pia napenda kutoa shukrani kwa wale wote waliokuwa wakisiliza salvation radio tz online kuwa matangazo hayo kwa sasa yamesimama rasmi.

Tutaonana tena  na kurudi hewani Mungu akipenda
salvation radio


asanteni sana nini mimi Gasper sambweti
0755 656445

sambweti@gmail.com

Wednesday, January 24, 2018

Kenya: Wanafunzi walipigana kwa kutumia visu kutokana na madai ya ubaguzi wa kidini

Shule ya Upili ya jamhuri iliopo mjini NairobiHaki miliki ya pichaJAMHURI/FACEBOOK
Image captionShule ya Upili ya jamhuri iliopo mjini Nairobi
Polisi nchini Kenya wanachunguza ghasia katika shule ya upili ya umma ambapo wanafunzi kadhaa walidungwa visu kutokana na madai ya ubaguzi wa kidini .
Ghasia za wanafunzi sio jambo geni lakini kile ambacho kimewawacha wengi mdomo wazi ni vile wanafunzi hao walivyofanikiwa kuingia katika shule hiyo wakiwa na visu na mapanga.
Kulingana na mwandishi wa BBC Mercy Juma shule ya upili ya Jamhuri iliopo katika mtaa wa jiji la Nairobi imefungwa mara moja na wanafunzi walio zaidi ya 1,500 kurudishwa nyumbani.
Haijulikani ni nini hasa kilichosababisha ghasia hizo za Jumanne usiku ambazo ziliwawacha wanafunzi saba na majareha katika vita vilivyohusisha visu na mapanga.
Mpango wa elimu bila malipo Tanzania umefanikiwa?
watoto waliokimbia kufanyiwa ukeketaji
Afisa mkuu wa jiji la Nairobi Japeth Koome anasema kuwa wameanzisha uchunguzi dhidi ya madai ya utaratibu wa kidini katika shule hiyo.
Vyombo vya habari nchini humo vina habari kwamba vita hivyo vilizuka baada ya baadhi ya wanafunzi kupinga kuhusu upendeleo wa kidini unaodaiwa kutekelezwa na wakuu wa shule hiyo.
Wakenya katika mitandao ya kijamii wameshangazwa na vile silaha kama vile visu na mapanga zilivyoingia katika shule hiyo.

Papa Francis: Majaribu ya nyoka kumdanganya Eve kula tunda katika biblia ni kisa cha 'habari bandia'

Papa Francis
Image captionPapa Francis
Papa Francis ameshutumu njia za udanganyifu miongoni mwa wale wanaosambaza habari bandia akisema kuwa kisa cha kwanza cha habari bandia kipo katika biblia wakati Eve alipohadaiwa na nyoka kula tunda lililokatazwa.
Kisa hicho kinaonyesha athari kali ambazo habari bandia zinaweza kusababisha, Papa Francis alionya katika nakala.
Francis amesema kuwa hatua hiyo ilisababisha kusambaa kwa chuki na kiburi.
Aliwataka watumizi wa mitandao ya kijamii na waandishi kutotumia njia ambazo zinaweza kusababisha migawanyiko.
Nakala hiyo kwa jina Ukweli utakuwacha huru, habari bandia na uandishi wa amani ilitolewa kabla ya kufanyika kwa siku ya mawasiliano ya kanisa hilo itakayofanyika tarehe 13 mwezi Mei, na ilikuwa mara ya kwanza Papa Francis kuandika kuhusu mada hiyo.
Mtoto amvua kofia Papa Francis
Amewataka watumizi wa mitandao ya kijamii na waandishi kukabiliana na njia za udanganyifu ambazo husababisha migawanyiko.
Inajiri huku kukiwa na mjadala wa njia za kukabiliana na habari bandia katika mitandao ya kijamii na vile zitakavyoshawishi uchaguzi wa hivi karibuni, ikiwemo Marekani 2016.
''Usambazaji wa habari bandia unalenga kuendeleza malengo fulani ,kushawishi maamuzi ya kisiasa na kuhudumia maslahi ya kiuchumi'', alisema Papa Francis
Akilinganisha na ujumbe wa majaribio katika biblia, aliongezea: Lazima tufichue njia ambazo zinaweza kuitwa za udanganyifu zinazotumika na wale wanaodanganya kwa lengo la kushambulia wakati wowote na eneo lolote lile.
Alitaka kuwepo kwa elimu kuhusu ukweli ambayo itawaelimisha watu kutambua kutathmini na kuelewa habari.
Aliongezea kwamba jukumu la waandishi ambao aliwaita walinzi wa habari sio kazi pekee bali ujumbe.
Alisema kuwa hawafai kuangazia sana habari mpya bali kutathmini maswala tata yanazua mizozo.

Wanaojidai kuwa manabii wanahubiri dini?


Mwanamume anayejiita Nabii TitoHaki miliki ya pichaHISANI
Image captionMwanamume anayejiita Nabii Tito

Kuelekeza waumini kula nyasi, kuwapulizia dawa za kuua wadudu machoni waumini kwa ahadi ya kupata utajiri, kupata uponyaji na kuuona ufalme wa Mungu ni miongoni mwa yale ambayo wamekuwa wakihubiri wale wanaojiita manabii ama watumishi wa Mungu barani Afrika.
Katika tukio la hivi karibuni nchini Tanzania Jeshi la polisi nchini humo linamshikilia mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Onsemo Machibya maarufu kwa jina alilojipa la Nabii Tito.
Mhubiri huyo anadaiwa kusambaza dini yake kupitia vipeperushi na picha za video, huku maudhui ya imani hiyo yakidaiwa kukinzana na maadili ya Kitanzania.
Jeshi la Polisi katika taarifa yake kwa vyombo vya habari lilisema mwanamume huyo ana matatizo ya akili na bado linaendelea kumshikilia.
Tito alijizolea umaarufu mitandaoni siku za hivi karibuni baada ya kusambaa kwa video zake kadhaa zikimuonyesha yeye na walioelezwa kuwa ni waumini wake wakinywa pombe wakati wa ibada yao lakini pia kucheza nyimbo mbalimbali hasa kwa kunengua viuno.
Kwenye moja ya video hizo, anaonekana kumbusu mdomoni aliyedaiwa kuwa mkewe pamoja na mwanamke mwingine anayedaiwa kuwa kijakazi wake.
Nabii Tito kwenye video hiyo anasema maandiko yameruhusu mwanaume kufanya zinaa na kijakazi wake.

Uhuru wa kuabudu una mipaka?

Padri Leons Maziku, ambaye ni mtaalamu wa Saikolojia na Mhadhiri katika chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino anasema kwa mujibu wa tamko la umoja wa maifa la mwaka 1948 kuna uhuru wa kuabudu lakini uhuru huo umewekewa mipaka kisheria.
Padri Maziku anasema uwepo wa manabii hawa kunawaondolea heshima na hadhi viongozi wa dini lakini pia watu hawa wanaojiiita manabiii wanawatesa watu kisaikolojia hasa pale wanapobaini kuwa waliyemfuata ni nabii wa uongo
Licha ya kupingwa na baadhi ya watu, wapo wale wanaoamini kuwa kila mtu ana uhuru wa kuabudu anachokitaka.
Hivi karibuni nchini Afrika ya Kusini nako serikali ya nchi hiyo ilimpiga marufuku kiongozi wa kidini ambaye alikuwa na tuhuma na zenye kuendana na hizo.